Millionaire  AdsAuthor Topic: MWALIMU MKUU WA SEKONDARI ILIYOONGOZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA KITAIFA AHAMA  (Read 944 times)

Offline mastory

  • Trade Count: (0)
  • Premium Sponsor
  • Full Member
  • ******
  • Posts: 192
  • Karma: +0/-0
  • Referrals: 4
    • View Profile
MKUU wa Shule ya Sekondari Igowele iliyopo katika kijiji cha Igowole, wilayani Mufindi Mkoani Iringa amelazimika kuhama nyumba yake ili kulinusuru kundi kubwa la wanafunzi wapya wa kike wa kidato cha tano waliopangiwa kujiunga na shule hiyo.

Igowole ambayo ni shule ya kata imeingia katika historia ya elimu nchini baada ya mwaka huu kuongoza kitaifa kwa kushika nafasi ya kwanza katika matokeo ya kidato cha sita.

Kati ya wanafunzi wake 30 waliomaliza elimu hiyo mwaka huu, 19 walipata daraja la kwanza (Division One), 10 daraja la Pili (division two) na mmoja alijipatia daraja tatu (Division three).

Kuondoka kwa mkuu wa shule hiyo, Andrew Kauta katika nyumba hiyo kutawawezesha jumla ya wanafunzi 30 kati ya 237 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano hivi karibuni, kupata makazi ya muda.

Kauta alisema hatarudi katika nyumba hiyo mpaka pale, tatizo la mabweni katika shule hiyo litakapopatiwa ufumbuzi.

“Ili kuwanusuru wanafunzi hawa, ni bora nikaishi katika nyumba yoyote kijijini; tunataka wanafunzi wote wa kidato cha tano na sita katika shule yetu wakae bweni,” alisema.

Wanafunzi wengine wataunga na wenzao 30 wa kidato cha sita mwaka huu katika bweni la muda mrefu lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 87 katika mazingira ya kubanana.

Watakaobaki, kwa mujibu wa Mwalimu wa Taaluma, Isiaka Chodota watatumia madarasa matatu kama mabweni yao ya muda.
Huyu mwalimu anastahili pongezi kwakweli
Click my link join I will tell you how to get money from this website, Join now http://www.chatguest.com/index.php?action=refferals;refferedby=15

Share on Facebook Share on Twitter


 


Millionaire  Ads
Millionaire  Ads
Never use defamatory language, Do not dare to disturb someones peace on this online Forum
 Copyright ©2016 Chatguest.com. All rights Reserved