MillionaireAdsAuthor Topic: Post za walimu 2016/2017 au ajira mpya za walimu 2016/2017 habari mpya hapa  (Read 30155 times)

Offline Support

 • Trade Count: (0)
 • Administrator
 • Hero Member
 • *****
 • Posts: 858
 • Karma: +0/-0
 • Hamia https://www.jamiihuru.com
 • Referrals: 3424
  • View Profile
Mada post za walimu 2016/2017 ipo hapa kujuzana habari na masuala ya ajira mpya za walimu mwaka 2016/2017. Hongera mwalimu uliyehitimu mafunzo ya ualimu mwaka 2015 na umeshapata matokeo ya ualimu 2015 sasa unasubiri post yako yaani kituo cha kazi hongera sana. Wengi walipenda wafikie hatua uliyoipiga lakini kutokana na sababu mbali mbali walishindwa lakini wewe kwa nguvu yako  na nguvu uliyopewa na Mungu umeweza kuwa mwalimu.
Jiunge na mtandao huu wa chatguest utumiwe taarifa kwenye email yako mara tu post za walimu zitakapokuwa zimetangazwa bonyeza hapa

Wakati ukisubiri kupangiwa kituo cha kazi unafanya nini mtaani? Usikae bure tu ukisubiri mpaka siku upangiwe shule ya kufundisha jaribu kutafuta ajira za muda kwenye shule za binafsi ili usiwe tegemezi sana kwa wazazi au walezi kama wewe ni kijana usiyejitegemea. Unaweza kufanya hata biashara wakati huu ukisubiri post za ualimu 2016/2017 Usikae bure vipo vitu vingi vya kufanya hata kuanzisha tuition mtaani kwako na kuanza kufundisha watoto huku ukijipa uzoefu zaidi wa kufundisha.


 Endelea kufuatilia post za walimu 2016/2017 au ajira mpya za walimu 2016/2017 hapa hapa chatguest.com mpaka zitakapotangazwa na idara husika yaani pmorlg na moe
Kumbuka kujiunga na mtandao huu utumiwe taarifa kwenye email yako mara tu post za walimu zitakapokuwa zimetangazwa bonyeza hapa


Niongee na wale ambao mpaka leo hii japo wamepata matokeo yao ya ualimu 2015 lakini moyoni bado wana dukuduku kuwa wakipangiwa kijijini hawaendi kuripoti. Walimu kama hawa hawajui wanalolifikiria. Chezea nafasi hiyo halafu utaona joto la jiwe. Kuwa na huruma kwa jamii inayoishi vijijini, wote tukikataa kwenda kufanya kazi vijijini wale watu watapataje elimu? Isitoshe wewe mwenyewe unaweza kuwa ulizaliwa kijijini pengine umekulia kijijini na umesoma kijijini kwa muda lakini leo unawasaliti wanaoishi vijijini na kusema huwezi kufanya kazi huko eti hakuna umeme hakuna huduma nzuri za kijamii acha zadharau kijana nenda karipoti kazini anza maisha pesa utalipwa na zitakusaidia kuboresha maisha huko kijijini uendako. Utaweza kununua hata solar power na kupata umeme kama wale waliopangiwa mjini kama hakuna maji utatumia baadhi ya pesa hata kuchimba kisima mtakachopata maji ya kutosha au kwa kutumia ubunifu mbalimbali mnaweza kuvuta maji toka vyanzo vya maji vya jirani mpaka shuleni kwenu.
Umeshajiunga na mtandao huu utumiwe taarifa kwenye email yako mara tu post za walimu zitakapokuwa zimetangazwa bonyeza hapa
Kijijini kuna raha zake kama utatumia ubongo wako kufikiri jinsi ya kutajirika kwa kutumia fulsa zilizopo kijiji. Unaweza kununua gari muda mfupi tu ukiwa huko kijijini tena bila hata ya kukopa ili uanze kurejesha mkopo kwa kukatwa kwenye mshahara wako. Kama kuna tatizo la usafiri basi wewe utakuwa wa kwanza kutatua tatizo hilo kwa kupeleka hata gari dogo la abiria litakalotumika kusafirisha abiria kutoka huko kijijini hadi mjini na kinyume chake.
Hakikisha unajiunga na mtandao huu utumiwe taarifa kwenye email yako mara tu post za walimu zitakapokuwa zimetangazwa bonyeza hapa

Tatizo la nyumba za walimu vijijini nalo si kikwazo cha wewe kutokwenda kuripoti kwani si kweli kwenye jamii yoyote hakuna nyumba, Pia kwakutumia ubunifu wako na mshahara utakaolipwa utaweza kujenga nyumba ya kuanzia maisha hata kama ni ndogo. Mwanzo mgumu lakini baada ya miaka huko kijijini utakuona mjini kwakua mahitaji yote utakayotaka unaweza kuyapata kwakua pesa zitakuwepo na wewe ndiye mtafutaji.
Jiunge na mtandao huu utumiwe taarifa kwenye email yako mara tu post za walimu zitakapokuwa zimetangazwa bonyeza hapa

Chukua mfano umeenda kijijini kuanza kazi kisha muda ule usio wa kazi ukajishughulisha kwenye shughuli za uzalishaji mali kama kilimo ufugaji au biashara kwa kutumia fulsa zinazopatikana hapo kijijini baada ya miaka michache tu wewe utakuwa mwalimu Tajiri hapo kijijini.

Wapo wanaowaza kuwa wao watafanya kazi ya ualimu kwa miaka miwili tu kisha wataenda kusoma na kubadili fani hiyo eti wakijidanganya hailipi mshahara mdogo au hawataki kuchafuka na vumbi la chaki wengine wanaenda mbali zaidi na kuiponda kazi ya ualimu wakisema wanaogopa kuugua kifua kikuu kutokana na vumbi la chaki. Kama mwalimu angekuwa anaugua kifua kikuu kutokana na vumbi la chaki basi watanzania wote tungekuwa tuna ugonjwa wa kifua kikuu kwakua kifua kikuu kinaambuizwa sasa wanafunzi wote darasani nao wangegoma kusoma kwakua wanaogopa kuambukizwa kifua kikuu pia wewe ulipokuwa mwanafunzi ungeugua kifua kikuu kwakua ulifuta ubao ulimkaribia mwalimu wako mara kadhaa. Hizo zote ni fikra potofu achana nazo kabisa, nenda kapige kazi ya ualimu itakulipa kuliko fani nyingine ambazo kupata ajira mpaka ukaoge maji ya mganga wa kienyeji.
Jiunge na mtandao huu utumiwe taarifa kwenye email yako mara tu post za walimu zitakapokuwa zimetangazwa bonyeza hapa
Mwisho kabisa mwalimu unakaribishwa kutumia mtandao huu bora kabisa wa kuelimishana mambo mbalimbali ya kijamii pia unaweza kuongeza kipato kwa kufundisha wanafunzi mada mbalimbali hapa mtandaoni na kulipwa. Cheza games na ulipwe pia unalipwa kwa kila mtu utakayemwambia atumie mtandao huu kwa kupata elimu. bonyeza hapa ufungue account dakika mbili tu na ni bure. Endelea kufuatilia post za walimu 2016/2017 au ajira mpya za walimu 2016/2017 hapa hapa chatguest.com mpaka zitakapotangazwa na idara husika yaani pmorlg na moe
Muhimu: Tangazo hakikisha umejisajiri kwenye mtandao wetu mpya wa kisasa ili ulipwe kila unapoandika makala kwenye mtandao huo Bonyeza link hii --> https://www.jamiihuru.com Ukiandika hapa chatguest huwezi kulipwa.

Share on Facebook Share on Twitter


Offline moses nyingi

 • Trade Count: (0)
 • Newbie
 • *
 • Posts: 5
 • Karma: +0/-0
 • Write something get paid. Invite friends get paid. Play games get paid. Create account click the link http://www.chatguest.com/index.php?action=register
 • Referrals: 0
  • View Profile
post za uwalimu zinatoka Lin?

Offline Support

 • Trade Count: (0)
 • Administrator
 • Hero Member
 • *****
 • Posts: 858
 • Karma: +0/-0
 • Hamia https://www.jamiihuru.com
 • Referrals: 3424
  • View Profile
Ukipata taarifa kuwa ajira za walimu 2016 zimetangazwa basi usikose kuwajulisha wanachama wa mtandao huu. Tupo wengi tunasubiri hizo ajira za walimu 2016
Muhimu: Tangazo hakikisha umejisajiri kwenye mtandao wetu mpya wa kisasa ili ulipwe kila unapoandika makala kwenye mtandao huo Bonyeza link hii --> https://www.jamiihuru.com Ukiandika hapa chatguest huwezi kulipwa.

 


Millionaire  Ads
MillionaireAds