Millionaire  AdsAuthor Topic: WASIO TOA CHAKULA KWA WANAFUNZI KWENDA JELA'  (Read 365 times)

Offline mastory

  • Trade Count: (0)
  • Premium Sponsor
  • Full Member
  • ******
  • Posts: 192
  • Karma: +0/-0
  • Referrals: 4
    • View Profile
WASIO TOA CHAKULA KWA WANAFUNZI KWENDA JELA'
« on: July 21, 2014, 09:00:50 pm »
HALMASHAURI ya Wilaya ya Sumbawanga mkoani Rukwa, imetoa siku 14 kwa watendaji wa vijiji kuhakikisha shule zilizopo katika vijiji vyao zinatoa chakula  cha mchana kwa wanafunzi, na atakayeshindwa awekwe ndani kwa siku saba.
Agizo hilo lilitolewa juzi na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Chrispin Luanda katika mkutano wa hadhara wakati akizungumza na wakazi wa Kijiji cha Kaengesa wilayani hapa wakati wa ukaguzi  wa utekelezaji wa sera ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Alibainisha kuwa halmashauri imelazimika kutoa agizo hilo kufuatia taarifa kuwa baadhi ya watendaji wa vijiji wamekuwa ni kikwazo kikubwa, ambapo wamekuwa wakikwamisha utekelezaji miradi ya maendeleo katika maeneo yao.
Aliongeza kuwa kutokana na baadhi ya watendaji wa vijiji kukaidi utekelezaji wa miradi ya maendeleo, sasa ni wakati muafaka kuanza kuwawajibisha wanaolegalega.
“Natoa siku kumi na nne kwa watendaji wa vijiji wote wahakikishe kuwa kuanzia sasa   wanafunzi wa shule zote za msingi wilayani humu wanapata chakula cha mchana shuleni, yeyote atakayeshindwa akamatwe na kuwekwa ndani kwa siku saba ili iwe fundisho si kwake tu bali pia kwa wengine wanaoendekeza  tabia hiyo,” aliagiza.
Luanda alieleza kuwa changamoto kadhaa zinazozikabili shule za msingi  wilayani humo zinaweza kutatuliwa, lakini tatizo kubwa ni baadhi ya viongozi wa serikali kutowajibika kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Naye Ofisa Elimu Shule za Sekondari wilayani hapa, Emiliana Fungo, alisema wazazi wanao wajibu wa kutatua changamoto za shule wanazosoma watoto wao ili matokeo bora yapatikane.
 Chanzo:Tanzani Daima
Click my link join I will tell you how to get money from this website, Join now http://www.chatguest.com/index.php?action=refferals;refferedby=15

Share on Facebook Share on Twitter


 


Millionaire  Ads
Millionaire  Ads
Never use defamatory language, Do not dare to disturb someones peace on this online Forum
 Copyright ©2016 Chatguest.com. All rights Reserved