Millionaire  AdsAuthor Topic: Mfahamu mwanzilishi na mmiliki wa mtandao wa chatguest.com  (Read 20 times)

Offline Support

  • Trade Count: (0)
  • Administrator
  • Hero Member
  • *****
  • Posts: 851
  • Karma: +0/-0
  • Hamia https://www.jamiihuru.com
  • Referrals: 3424
    • View Profile
Mfahamu mwanzilishi na mmiliki wa mtandao wa chatguest.com
« on: August 23, 2016, 03:12:34 pm »
Mara nyingi tumekuwa tukitumia mitandao ya kijamii bila kujiuliza ni nani mmiliki wa mtandao huo. Ukiulizwa swali taja jina la mmiliki wa mtandao wa facebook unaweza ukashindwa kutaja lakini kila siku ya mungu unatumia facebook.

Hivyo hivyo ukiulizwa nani ni mmiliki wa mtandao wa google unaweza usitaje jina lake wakati toka kidato cha kwanza mpaka chuo kikuu unatumia google kupata habari na kujifunza.

Nataka usishindwe kumtaja mwanzilishi wa mtandao wa chatguest.com mtandao unaopendwa na watu wengi kwakua mtandao huu unakulipa ukiandika makala za kufundisha jamii au kuelimisha jamii kwa lugha nyingine. Mtandao huu wa chatguest.com unakulipa ukicheza games hapa online na kuapata alama zilizopangwa. mfano kama gemu lako unalipwa ukifikisha score 100 basi cheza mapaka upate score 100 kisha wasiliana na moderators wakulipe pesa zako pia mtandao wa chatguest.com unakulipa ukialika marafiki watumie mtandao wa chatguest.com.

Mfahamu mmiliki wa mtandao huu kwa majina aliyopewa na wazazi wake na elimu yake pia utajua wapi anaishi kwa sasa na anafanya kazi gani.

Mr Mbena Riziki ndiye mmiliki wa mtandao wa chatguest.com alianzisha mtandao huu rasmi mwaka 2013 september. Kabla hajazindua mtandao huu alikuwa anamiliki blog za kawaida sana. alianza kutengeneza blog akiwa mwaka wa kwanza chuo kikuu cha kilimo sokoine Morogoro (SUA) anasema kutengeneza blog kwake ni hobby au interest alikuwa anafanya kazi hii hata akiwa chumba cha mazoezi ya kujifunza kompyuta Computer laboratory na library na Library ya chuo cha SUA. Alipenda sana kudesign website japo hakusomea Website designing course ujuzi alionao ni wa kutumia kompyuta kwenye intaneti hapo humdanganyi kitu.

Ukimpa mtihani wa kutafuta taarifa kwenye intaneti lazima apate alama 100 na atawashinda hata wanafunzi waliosomea Information technology moja kwa moja. Pia kwenye maswala ya kucheza na html codes na java scripts hapo ndio mahala pale hata aje mwanafunzi aliyosomea website designing hapa kwa mr Mbena lazima asalimu amri.

Mr mbena kama nilivyoeleza hapo juu amesoma chuo kikuu cha sua na kuhitimu degree ya kwanza mwaka 2011 amefanikiwa kuajiriwa serikalini anafanya kazi serikali za mitaa katika wilaya mpya ya buhigwe. Wanabuhigwe mmepata jembe kompyuta zenu zikisumbua kijana mnaye hapo. Ametoa zawadi kwa wanabuhigwe kwa kuanzisha blog inayoitwa buhigweyetu.blogspot.com. Mr mbena ni mtaalamu wa maendeleo ya jamii lakini kwa chuo cha SUA ukisomea biashara basi lazima wewe ujue IT wewe ujue udaktari wa mifugo japo kwa kiasi kidogo.
Amesomea maendeleo ya jamii lakini ndani yake ni mtaalamu wa kompyuta mtaalamu wa ujasiriamali na mambo mengine.

Mr mbena ni mzaliwa wa mkoa wa Iringa lakini makazi yake ya kudumu yapo Manispaa ya Morogoro.
Mafanikio aliyoyapata kupitia mtandao wa chatguest.com

1. Mr mbena ameweza kununua kiwanja mjini morogoro chenye thamani ya Tsh 2,500,000 ukubwa wa 560 squire metre  ambacho anataka afungue mradi wa ufugaji nyuki maeneo ya kiegea kihonda. Hii ni kutokana na pesa alizopata kupitia mtangazo yanayowekwa chatguest.com toka mtandao uanze.

changamoto Mr mbena anasema kila chenye faida hakikosi changamoto. katika kuanzisha mtandao wa chatguest kama isingekuwa ni interest au hoby basi angekata tamaa mapema sana yaani miezi michache toka afungue mtandao huu. Kwakua anafanya kitu anachokipenda hii imemfanya asikate tamaa, Anasema unapoanzisha mtandao kama huu wa kijamii kuna changamoto kubwa ya kupata watu watakaojisajiri kwenye mtandao wako na kuendelea kuutumia mtandao wako. kadili wanavyoutumia mtandao wako ndivyo unavyoingiza mapato mengi. Sasa anasema alipofungua mtandao huu alitumia pesa kama dola 200 kufanya usajiri wa jina na huduma nyingine za msingi za kuufanya mtandao uweze kuwepo hewani sasa akajikuta watu hawajisajiri kama alivyotegemea na hakuna matangazo anayopokea toka kwa watembeleaji wake takribani kwa muda kama wa mwaka mzima. hapo kijana kama si hobby lazima ukate tamaa na kuuacha mtandao bila matunzo hatimaye mtandao wako unakufa. Mr mbena hakukata tamaa aliendelea kuutangaza mtandao wa chatguest.com kwenye google na facebook mpaka leo mtandao huu unawanachama hai 7330 mpaka tarehe ya taarifa hii kuandikwa.

Changamoto nyingine ni mwitikio mdogo wa vijana kuandika makala nzuri hapa mtandaooni wengine wakidhani wanadanganywa labda hakuna malipo lakini Mr mbena anasema yeye alisoma kidato cha kwanza mpaka cha nne shule ya seminary Mafinga hivyo alitarajiwa kuwa mhubiri kanisani yaani Padre lakini mungu alikuwa na malengo naye tofauti kidogo hivyo hawezi tapeli vijana hapa mtandaoni. Nafsi yake itamsuta. Anasisitiza vijana mnaopoteza muda facebook na whats app tumieni fulsa hii hapa chatguest.com mpate mitaji ya kuanzishia biashara zenu binafsi msilalamike hakuna ajira bali nyie tafuteni mitaji kupitia chatguest.com kisha anzisheni biashara zenu na mtengeneze ajira kwa wengine.

Hapa chatguest kuna fulsa tatu za msingi ambazo ukizingatia lazima utoke na kitita cha pesa. Kuna kulipwa ukicheza games online, kuna kulipwa ukiandika makala na kuna kulipwa ukialika marafiki wajiunge na chatguest.com. Waite watoke huko waliko wanapoteza muda waje hapa wanufaike pamoja nawe.

Kwa leo napenda kumtambulisha mmiliki wa mtandao wa chatguest.com kama nilivyoeleza hapo juu

 pichani ndiye yeye
Muhimu: Tangazo hakikisha umejisajiri kwenye mtandao wetu mpya wa kisasa ili ulipwe kila unapoandika makala kwenye mtandao huo Bonyeza link hii --> https://www.jamiihuru.com Ukiandika hapa chatguest huwezi kulipwa.

Share on Facebook Share on Twitter


 

Related Topics

  Subject / Started by Replies Last post
1 Replies
40 Views
Last post April 11, 2016, 06:06:20 pm
by jimmy22
0 Replies
46 Views
Last post July 22, 2016, 10:39:27 am
by Support
3 Replies
44 Views
Last post August 20, 2016, 02:30:35 pm
by judge
0 Replies
28 Views
Last post September 15, 2016, 07:19:02 pm
by Support
0 Replies
13 Views
Last post September 20, 2016, 08:18:22 am
by Support

Millionaire  Ads
Never use defamatory language, Do not dare to disturb someones peace on this online Forum
 Copyright ©2016 Chatguest.com. All rights Reserved